Mtaalamu wa OECD: Ufufukaji wa uchumi wa China ni muhimu kwa dunia nzima
2020-11-26 19:20:05| CRI

Mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera za China katika Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) Bibi Margit Molner amesema China ikiwa ni nchi kubwa ya pili kiuchumi duniani, uchumi wa China unatangulia kufufuka baada ya kujikwamua kutoka kwenye athari za janga la virusi vya Corona, hali ambayo ina maana kubwa kwa dunia nzima.

Bibi Molner amesema, China siku zote imekuwa ikiunga mkono mapambano ya kimataifa dhidi ya virusi vya Corona, na kutoa misaada mingi ya vifaa tiba kwa nchi zenye mahitaji. Ameongeza kuwa kutokana na uchumi wa China kuendelea kufufuka, China si kama tu itaendelea kutoa bidhaa zinazohitajika kwa nchi nyingine, bali mahitaji ya China kwa malighafi na bidhaa kutoka nchi za nje pia yataongezeka hatua kwa hatua, hali ambayo ni muhimu kwa ufufukaji wa uchumi wa dunia.