Rais wa China ampongeza Bw. Biden kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani
2020-11-26 09:10:38| CRI

Rais Xi Jinping wa China Jumatano amemtumia Bw. Joe Biden ujumbe wa kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani. Rais Xi amesema, kukuza maendeleo yenye ustawi na utulivu wa uhusiano kati ya China na Marekani si kama tu kunaambatana na maslahi ya kimsingi ya wananchi wao, bali pia kunaendana na matarajio ya pamoja ya jamii ya kimataifa. Rais Xi amezitaka nchi hizo mbili zishirikiane na nchi nyingine pamoja na jumuiya ya kimataifa kuhimiza majukumu makubwa ya amani na maendeleo ya dunia.