UM watoa dola milioni 25 za kimarekani kwa miradi inayoongozwa na wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia
2020-11-26 09:11:51| CRI

Umoja wa Mataifa umetoa dola milioni 25 za kimarekani kutoka mfumo wa dharura kuunga mkono mashirika yanayoongozwa na wanawake ambayo yanazuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia. Fedha hizo zimetolewa kwa Mfuko wa Watu wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Wanawake la Umoja huo, na zaidi ya asilimia 30 ya fedha hizo zitatumika kusaidia mashirika yanayoendeshwa na wanawake ambayo yanalenga kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, kuwasaidia waathirika kupata huduma za matibabu, uzazi wa mpango, ushauri wa kisheria, mahali penye usalama, huduma za afya ya kisaikolojia na ushauri.