Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon atoa mwito kwa Umoja wa Ulaya kuisaidia kutatua mgogoro wa ndani
2020-11-27 19:31:40| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon Bw. Charbel Wehbe jana alisema, Lebanon inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kifedha na kiuchumi, na inahitaji kuimarisha ushirikiano kati yake na Umoja wa Ulaya, anatumai Umoja wa Ulaya utaiunga mkono kwenye nyanja mbalimbali.

Katika mkutano wa mawaziri wa Umoja wa Ulaya na nchi jirani za kusini uliofanyika kwa njia ya video, Bw. Wehbe ametoa mwito wa kuimarisha uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na nchi jirani za kusini, kuhimiza mazungumzo kati ya staarabu na tamaduni tofauti. Pia ametetea kujenga uhusiano wa wenzi wa kusaidiana katika suala la wahamiaji na nishati.

Amesisitiza kuwa, usalama na utulivu katika eneo la Bara Arabu ni muhimu sana. Migogoro isiyosita katika eneo hilo, na wakimbizi wengi wanaoingia nchi za Ulaya na nchi nyingine, vimesababisha hali ya usalama wa jamii na uchumi katika nchi zilizowapokea kuwa mbaya zaidi.

Amesema Lebanon inajitahidi kuimarisha ushirikiano kati yake na Umoja wa Ulaya, na kutumai Umoja wa Ulaya utaisaidia kukabiliana na changamoto, ili kutoa ufumbuzi endelevu wa suala la wakimbizi na wahamiaji haramu.