China na Afrika zafanya juhudi kwa pamoja kujenga makazi mazuri ya masikilizano kati ya binadamu na mazingira
2020-11-27 09:04:08| CRI

Kituo cha Ushirikiano wa Mazingira kati ya China na Afrika kilizinduliwa hivi karibuni hapa Beijing.

Akizungumzia uzinduzi huo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema hii ni hatua nyingine muhimu ya utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Beijing mwaka 2018. Amesema China inapenda kuendelea kushirikiana na Afrika kusisitiza njia ya kujiendeleza kwa kuhifadhi mazingira, kutumia kaboni kwa kiwango cha chini, kuhifadhi milima na maji na viumbe hai, ili pande hizo mbili ziwe makazi mazuri ambayo mwanadamu anaishi na mazingira kwa masikilizano.