Waziri mkuu wa Uingereza aonya kufunga nchi kwa mara ya tatu
2020-11-27 18:15:26| cri

Waziri mkuu wa Uingereza aonya kufunga nchi kwa mara ya tatu

Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson ameonya uwezekano wa kufunga nchi kwa mara ya tatu mwakani, kama nchi hiyo ikilegeza zuio dhidi ya kuenea kwa virusi vya Corona.

Kabla ya hapo waziri wa afya wa Uingereza Bw. Matt Hancock alisema, nchi hiyo itaanza zuio la ngazi mpya ya tatu ili kupambana na COVID-19 baada ya kumalizika kwa amri ya kufunga nchi kwa mara ya pili kwa mwezi mmoja, wiki ijayo.

Habari zinasema, hivi sasa, Uingereza imeripoti watu 1,578,429 wenye COVID-19 na vifo 57,128.