SOKA: Aggrey Morris aagwa kwa mbwembwe Taifa Stars
2021-01-13 18:00:15| cri

Beki wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Aggrey Morris (36) ameagwa rasmi kuichezea Taifa Stars baada ya kuomba kustaafu timu ya taifa. Morris ameagwa kwa kucheza mchezo wake wa mwisho Taifa Stars wa kirafiki dhidi ya Congo DR na aliweza kutumia dakika 2 kwenye mchezo huo ikiwa ni mara yake ya mwisho kutumika ndani ya Stars baada ya kuomba kustaafu.

Hata hivyo Morris alikabidhiwa mfano wa hundi ya Tsh milioni 5 na jezi iliyosainiwa na wachezaji wote wa Taifa Stars kama sehemu ya kumuaga kwa utumishi wake wa muda wote Taifa Stars.