Naomi Campbell Kupigia Debe Utalii Kenya
2021-01-13 19:29:50| cri

Wizara ya utalii nchini Kenya imemteua mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell kama balozi wa kimataifa wa Magical Kenya.

Akitoa tangazo hilo  Waziri wa Utalii na Wanyamapori Najib Balala alisema kuwa Campbell alipewa jukumu la kustawisha Kenya kama utalii bomba na kusafiri duniani.

Katika ripoti, wizara hiyo ilisema kuwa kuteuliwa kwake kulifikiwa baada ya mkutano kati ya msanii huyo na Bw Balala.

Mwanamitindo  huyo alikuwa Kenya katika likizo yake huku akiishi katika nyumba ya mapumziko huko pwani.