Rais wa Botswana awataka wanafunzi wafuate hatua za kukinga COVID-19
2021-01-13 09:20:53| cri

 

 

Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana jana amewataka wanafunzi waimarishe hatua za kujikinga na COVID-19, wakati muhula mpya wa masomo wa mwaka 2021 ukianza nchini humo.

 Rais Masisi amewataka wanafunzi kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi, kuweka umbali wa kijamii na kuvaa barakoa, na kuongeza kuwa serikali yake itafanya juhudi kuhakikisha usalama wa wanafunzi, pia amewataka wazazi na wanafunzi wafuate hatua husika.

Botswana imechukua hatua kadhaa ili kuzuia maambukizi ya COVID-19 shuleni, ikiwemo kupunguza idadi ya wanafunzi darasani, kuajiri wafanyakazi zaidi, na kukarabati vituo vya kunawia mikono.