Shilingi ya Uganda yaporomoka dhidi ya dola ya Marekani
2021-01-14 19:26:14| cri

Kuongezeka thamani kwa dola ya Marekani duniani kumesababisha thamani shilingi ya Uganda kuanguka kwa asilimia 0.3 katika siku tatu zilizopita.

Mbali na kuimarika kwa dola ya Marekani duniani,washiriki wa masoko katika soko la fedha na Benki ya Uganda wanasema kuwa kuna ongezeko la hitaji la dola kutoka kwa wawekezaji.

Nchini Uganda,viwango vya ubadilishanaji fedha vinasasishwa mara tatu kwa siku huku viwango tofauti vikitajwa,ambavyo huenda vikawa juu au chini,vikiashiria kupanda au kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine katika soko.

Kufikia jana mchana,kiwango rasmi cha uabdilishaji fedha kilichotolewa na Benki ya Uganda kilionyesha kuwa shilingi ya Uganda ilibadilishwa kwa Shs3,708.87 dhidi ya dola ya Marekani.