UM kutafiti ongezeko la kima cha maji katika maziwa nchini Kenya
2021-01-14 08:57:59| CRI

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Kenya, Walid Badawi amesema, Umoja huo utashirikiana na Kenya kutafiti ongezeko la kima cha maji kwenye maziwa nchini humo.

Akizungumza jijini Nairobi jana, Bw. Badawi amesema, katika siku za karibuni, Ziwa Baringo, Ziwa Naivasha na sehemu ya Ziwa Victoria zimeshuhudia hatari ya ongezeko la kima cha maji, ambalo limezamisha nyumba na kuathiri maisha ya watu.

Amesema, katikati ya mwezi Mei mwaka jana, Ziwa Victoria, ambalo ni kubwa zaidi barani Afrika, lilifikia kima cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa, na kusababisha miji na vijiji vilivyo kando yake kuzama.