China yachangia maendeleo duniani kwa kuhimiza ushirikiano wenye kiwango cha juu
2021-01-14 16:41:34| CRI

Waraka wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Maendeleo wa China katika Zama Mpya uliotolewa hivi karibuni umefafanua mawazo na mapendekezo ya China kuhusu ushirikiano wa kimataifa katika kuhimiza maendeleo. Wataalamu wanaona kuwa China kuhimiza ushirikiano huo kwa utulivu si kama tu itanufaisha nchi nyingine zinazoendelea duniani, bali pia itajinufaisha yenyewe.

Waraka huo unasema, China imeongeza ushirikiano wa kimataifa wa maendeleo kwa utulivu, na kutoa kipaumbele kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zaidi barani Asia na Afrika, na nchi zilizojiunga na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Mtafiti wa Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya China Teng Jianqun anasema,

“Madhumuni ya kutoa waraka huo ni kujulisha maendeleo na ushirikiano wetu yametoka wapi na yanakwenda wapi. Tumetoa kipaumbele kwa nchi zinazoendelea pamoja na nchi zilizojiunga na ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ katika ushirikiano huo. Sasa tuko kwenye jukwaa muhimu la kuongoza mambo ya kimataifa, hivyo kuzidisha ushirikiano wa kimataifa si kama tu kutazinufaisha nchi za kikanda na nchi nyingine zinazoendelea, bali pia kutainufaisha na China yenyewe.”

Kwa mujibu wa waraka huo, kuanzia mwaka 2013 hadi 2018, China imetoa misaada ya fedha zaidi ya Yuan bilioni 270, sawa na dola za kimarekani zaidi ya bilioni 41.7 kwa nchi za nje na mashirika ya kimataifa, haswa kwa miradi ya huduma za jamii, ushirikiano wa nguvukazi na teknolojia, mfuko wa ushirikiano kati ya nchi za Kusini, na misaada ya kibindamu ya dharura. Nchi zilizopata misaada ya fedha ya China ni pamoja na nchi 53 za Afrika, 30 za Asia, 22 za Latin-America na Caribbean, 9 za Oceania na 8 za Ulaya.

Waraka huo unasema, katika siku za baadaye, China itaendelea kufanya ushirikiano wa kimataifa wa maendeleo kadiri iwezavyo, ili kuchangia maendeleo duniani. Teng anasema,

“China inapenda kushirikiana na nchi zote ambazo bila kujali ni nchi zinazoendelea au nchi zilizoendelea. Kwani katika kijiji cha dunia, nchi zote zinapaswa kushirikiana ili kukabiliana na changamoto za pamoja. Katika siku za baadaye, China ikitaka kujiendeleza ziadi haiwezi kujitenga na dunia, wakati huohuo, maendeleo ya dunia pia yanahitaji mchango wa China.”

Teng amesema ili kuhimiza ushirikiano wa kiwango cha juu katika kuhimiza maendeleo duniani, China inatakiwa kuimarisha zaidi ushirikiano halisi kwa kufuata taratibu zilizopo tayari liikiwemo pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.