Rwanda-Wauzaji chakula walalamikia uhaba wa bidhaa
2021-01-14 19:28:02| cri

Wiki moja tangu serikali ya Rwanda ipige marufuku utembeaji kutoka wilaya moja hadi nyingine ,ndani na nje ya jiji la Kigali ,wauzaji chakula wameeleza wasiwasi wao kutokana na kupungua kwa usambazaji.

Manasseh Twizerimana ambaye anauza bidhaa za kuku katika soko la Kimironko anasema kuwa tangu uamuzi huo wa kusitisha utembeaji ulipotolewa,kuna  wafanyabiashara ambao nao waliamua kusimamisha biashara zao.

Alieleza kuwa kabla ya agizo hilo,wafanyabiashara wanaofanya biashara kama yake walikuwa wakikusanyika pamoja na kusafiri hadi mkoa wa Mashariki ambako walinunua kuku kwa wingi halafu kwa pamoja walikodisha gari na kusafirisha kuku hao hadi mjini Kigali.

Hata hivyo,anasema kuwa agizo hilo linamaanisha kuwa kupeleka kuku mjini Kigali imekuwa changamoto kwa sababu malori ambayo yanaruhusiwa katika njia hizo ni ghali mno na mara nyingi yanafanya biashara kubwa kubwa.

Twizerimana anasema kuwa agizo hilo sio tu limeathiri bei lakini pia limepunguza idadi ya wateja.