Kampuni ya Uingereza kutumia dola za kimarekani milioni 150 kuchimba gesi asilia katika bahari ya Israel
2021-01-15 09:02:42| CRI

Kampuni ya mafuta na gesi asilia ya Energean yenye makao makuu nchini Uingereza, imetangaza kuwa itatumia dola za kimarekani milioni 150 katika kuendeleza eneo la kuchimba gesi asilia la Karish Kaskazini kwenye bahari ya Mediterranean, katika pwani ya kaskazini nchini Israel. Kampuni hiyo inakadiria kuwa eneo la Karish Kaskazini lina hifadhi ya mita za ujazo bilioni 32 za gesi na mapipa milioni 34 ya mafuta, na uzalishaji kwenye eneo hilo unatarajiwa kuanza nusu ya pili ya mwaka 2023.