Wakenya Kuumia zaidi Bei Ya Mafuta Kipanda Tena
2021-01-15 19:23:58| cri

Wamiliki wa magari ya uchukuzi wa umma na ya kibinafsi watagharimika zaidi baada ya Mamlaka ya Kudhibiti Bei ya Kawi na Petroli (EPRA) kuongeza bei ya mafuta kuanzia siku ya Ijumaa.

Kwenye taarifa, EPRA ilisema kuwa bei ya petroli ya supa, dizeli na mafuta taa itaongezeka kwa senti 17, Sh4.57 na Sh3.56 mtawalia kwa kila lita.

Hii inamaanisha kwamba waliowekeza katika sekta ya uchukuzi pamoja na Wakenya wengi wanaotumia mafuta taa watagharimika zaidi kununua mafuta kwa bei mpya hadi Februari 14.

Hapo awali, bei ya petroli ya supa ilikuwa Sh106.82, dizeli Sh91.82 na mafuta taa Sh83.56 kwa Wakenya wanaoishi jijini Nairobi. Kutokana na mabadiliko hayo, petroli ya supa sasa itauzwa Sh104.60 mjini Mombasa, dizeli itauzwa kwa Sh94.01 huku Mafuta taa ikiwa Sh87.08 mjini humo.