Uagizaji wa mazao ya kilimo China kutoka Afrika waongezeka kwa miaka 4 mfululizo
2021-01-15 09:36:10| CRI

Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng jana alisema kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Novemba mwaka jana, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 167.8, huku thamani ya mazao ykilimo yaliyoagizwa na China kutoka Afrika ikiongezeka kwa asilimia 4.4 kwa miaka 4 mfululizo.

Bw. Gaofeng amesema, kutokana na athari za janga la COVID-19, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika unakabiliwa na changamoto kubwa, na katika hali hiyo China siku zote imekuwa ikisimama bega kwa bega na nchi za Afrika na kujitahidi kuendeleza ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali kwa nguvu na imani thabiti.