China yasema mawasiliano rasmi kati ya Marekani na Taiwan ni changamoto kwa kanuni ya China moja
2021-01-15 08:53:46| CRI

Msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan katika Baraza la Serikali la China, Zhu Fenglian ameeleza kupinga vikali mawasiliano rasmi kati ya Marekani na eneo la Taiwan la China, akisema hatua hiyo ni changamoto kwa kanuni ya China moja.

Zhu Fenglian amesema hayo alipojibu swali kuhusu mawasiliano yaliyofanyika jana alhamis kwa njia ya video kati ya Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Kelly Craft na kiongozi wa Taiwan, Tsai Ing-wen. Amesema kuna China moja tu duniani, na Taiwan ni sehemu ya China, hivyo kuitaka Marekani kushikilia kanuni ya China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani.

Pia ameutaka uongozi wa chama cha Democratic Progressive cha Taiwan kuacha mara moja aina yoyote ya ushirikiano na Marekani.