Hatua ya duka moja kumbandikia mzee karatasi yenye maneno “mimi ni mwizi” yazusha majadiliano makali
2021-01-19 21:03:51| cri

Hivi karibuni wanamtandao wamesema mzee mmoja alikuwa akitembea ndani ya duka moja kubwa akiwa na karatasi iliyoandikwa “Mimi ni mwizi”. Inaripotiwa kuwa mzee huyo alikamatwa na wafanyakazi wa duka hilo kwa kuiba vitu, na wafanyakazi walimwadhibu mzee huyo kwa kwa kitendo hicho. Katika video iliyosambazwa kwenye mtandao wa Internet, imeelezwa kuwa mzee huyo hatawajibishwa kama atatembea ndani ya duka hilo akiwa amebandikwa karatasi iliyoandikwa “mimi ni mwizi”.

Video hiyo imezusha gumzo miongoni mwa wanamtandao. Baadhi ya watu wanaamini kuwa wezi wanatakiwa kuadhibiwa kwa kuchukuliwa hatua kama hii, ili wengine watamabue aibu hiyo na kuacha wizi. Wanaopiga wanaamini kuwa ingawa wanaelewa hasira ya duka hilo, lakini hawaungi mkono kitendo hicho kwani kimemdhalilisha mzee, kudhuru haki yake na kukiuka sheria.