China kusaini makubaliano ya biashara huria pamoja na wenzi wengi zaidi wa biashara
2021-01-22 09:23:29| cri

Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng jana kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, China inapenda kusaini makubaliano ya biashara huria pamoja na wenzi wengi zaidi wa biashara, pia inazingatia kujiunga na makubaliano ya CPTPP.

Bw. Gao amesema mwaka 2020 nchi 15 ikiwemo China zilisaini rasmi makubaliano ya RCEP, na mwisho wa mwaka jana mazungumzo ya Mkataba wa Uwekezaji (BIT) kati ya China na Ulaya yamekamilika kwa utaratibu.

Bw. Gao amesema China itaendelea kupanua mtandao wa biashara huria. Vilevile China itafanya juhudi kuinua kiwango cha makubaliano ya biashara huria, na kufungua mlango zaidi kwa kiwango cha juu zaidi.