Gazeti la Renminribao: Kuagiza vyakula kwa kutumia simu ya mkononi haipaswi kuwa chaguo pekee kwa watumiaji
2021-02-02 20:45:26| cri

Kwa mujibu wa Gazeti la Renminribao, hivi sasa mikahawa mingi inatoa “huduma zisizo na mawasiliano kati ya watu”, ambapo watumiaji wanaweza kuagiza chakula na kulipa kwa njia ya kusoma nambari ya QR kwenye simu ya mkononi, hatua ambayo inarahisisha baadhi ya watumiaji na pia kuleta matatizo kwa wengine.

Bibi Jia mwenye umri wa miaka 40, alisema yeye si mtu wa kizamani ambaye anapenda kutumia njia mpya za kulipa, lakini uzoefu wa kuwasiliana na wahudumu, na kuchagua vyakula anavyovipenda, hauwezi kubadilishwa kwa kuagiza kwa nambari ya QR. Anaona kuwa njia ya kuagiza vyakula kwa kutumia simu ya mkononi inaharibu mawasiliano kati ya watu.

Imeripotiwa kuwa baadhi ya wazee pia wana shida ya kuagiza vyakula kwa kutumia simu ya mkononi, na wengine hawapendi kutumia njia hiyo kwa kuwa wana wasiwasi wa kuvujishwa taarifa zao kibinafsi.