Duka moja lawaajiri wafanyakazi kwa mshahara wa dola za kimarekani 1,500 kwa mwezi
2021-02-02 20:44:16| cri

Hivi karibuni tangazo la kuwaajiri wafanyakazi wa duka la mikate inayopikwa kwa mvuke bao zi mjini Hangzhou na kuwalipa mshahara wa dola za kimarekani 1,500 kwa mwezi linafuatiliwa na watu.

Tangazo hilo linasema, duka hili linataka kuwaajiri wafanyakazi hodari wawili, na kuwalipa mshahara wa zaidi ya dola za kimarekani 1,500, tena wataandaliwa chakula na makazi.

Mmiliki wa duka hilo Bw. Chen Xing anasema, ameandaa tangazo hilo kwa sababu wafanyakazi wawili waliondoka hivi karibuni, na kwamba anaweka masharti ya kufanya kazi kwa kiwango cha juu na kulipa mshahara mkubwa.

Bw. Chen Xing ana masharti matatu kwa wafanyakazi wa kutengeneza bao zi: kwamza kuzingatia usafi, pili kuweza kushirikiana na wenzake, na tatu kufanya kazi kwa bidii. Pia amesema malipo yatakuwa ni mshahara wa msingi wa dola 1200 pamoja na bonasi, na kwa jumla kwa kawaida wafanyakazi wote wanaweza kupata malipo zaidi ya dola elfu 1500. 

Kwa kweli mshahara mkubwa unategemea kazi ngumu. Bw. Chen Xing pia amesema isipokuwa wahudumu wa baa, wafanyakazi wengine wako kazini mwaka mzima bila ya kupumzika. Wakitaka kupumzika, wanapunguziwa dola 40 kwa siku. Kwa hivyo wafanyakazi hawataki kupumzika.