Mabavu ya aina yoyote hayaruhusiwi kwenye elimu nyumbani
2021-02-04 15:45:03| cri

Mswada wa Sheria ya Elimu ya Nyumbani uliwasilishwa tarehe 20 mwezi huu kwenye mkutano wa kamati ya kudumu ya Bunge la umma la China ili ujadiliwe. Mswada huo umeagiza kuwa wakati wazazi au wasimamizi wengine wa watoto wanapotoa elimu kwa watoto nyumbani, hawatakiwi kuwabagua kutokana na jinsia au hali yao ya kiafya, hawaruhusiwi kutumia mabavu ya aina yoyote, na wala hawatakiwi kuwalazimisha, kuwashawishi, kuwakubali au kuwatumikisha watoto kwenye shughuli yoyote inayokiuka sheria au maadili ya jamii.

China inapanga kutunga sheria inayoruhusu uingiliaji wa kiusimamizi kwa Elimu ya Nyumbani endapo kuna ulazima. Mswada huo unaona elimu ya nyumbani si kama tu ni mambo ya ndani ya familia, bali pia inahusiana na maslahi ya jamii, na pia umeweka bayana kuwa idara ya usalama wa umma, idara ya kuendesha mashtaka, na mahakama zina mamlaka ya kuingilia elimu ya nyumbani wakati zinapolazimika, pamoja na hatua watakazochukua kisheria kwenye uingiliaji huo.