Utaratibu wa kuwaadhibu “wasanii wenye maadili mabaya” watangazwa rasmi
2021-02-09 16:50:44| cri

Kanuni ya usimamizi wa wasanii wa sanaa za maonesho iliyotungwa na Shirikisho la wasanii wa sanaa za maonesho nchini China imetolewa rasmi hivi karibuni. Wasanii wanaopewa adhabu ya kufungiwa pamoja akitaka kuendelea kushiriki kwenye shughuli za maonesho, wao wenyewe au mashirika wanayofanya kazi wanatakiwa kuwasilisha ombi kwenye kamati ya maadili ndani ya miezi mitatu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kufungiwa, halafu kamati hiyo itatoa uamuzi baada ya kutathmini na kujadiliana.

Kwa mujibu wa kauni hiyo, wale wasanii waliokiuka kanuni na maadili, Shirikisho la Wasanii wa Sanaa za Maonesho litawapatia adhabu za aina tofauti kulingana na makosa yao, ikiwemo kuwakosoa na kuwaelimisha; kuwapiga marufuku kushiriki kwenye mashindano mbalimbali ya kugombea sifa, tuzo au ufadhili ndani ya sekta hiyo; kuwafungia kuanzia mwaka mmoja hadi maisha yote; na kushirikiana na mashirikisho ya sekta nyingine katika kuwasusia kwa pamoja.

Kutolewa na kutekelezwa kwa kanuni hiyo kunalenga kuwahimiza wasanii kuheshimu sheria, kanuni na maadili ya kijamii kwenye utendaji kazi na mienendo ya maisha, ili kujenga na kuelekeza maadili mazuri kwenye sekta ya sanaa za maonesho na katika jamii kwa ujumla.