SOKA: Messi kwenda PSG
2021-02-17 16:12:24| CRI

Kocha wa Barcelona, Ronald Koeman amesema uvumi kuwa nyota wa timu hiyo Lionel Messi kuhususishwa na kujiunga na klabu ya PSG haujawayumbisha kwa namna yoyote, licha ya mchezaji huyo kutaka kuondoka klabuni hapo mwishini mwa msimu huu. Mjustakabali wa Messi kubaki kwenye timu hiyo umekuwa na utata siku za karibuni, na PSG imekuwa ikitajwa kama timu ambayo huenda ikamchukua nyota huyo kama ataondoka Nou Camp katika dirisha kubwa la usajili.