Uganda: Wafanya biashara wapata muda zaidi kulipa mikopo
2021-02-17 17:31:58| CRI

Benki kuu ya Uganda imeongeza Hatua za Usaidizi wa Mikopo (CRM) kwa miezi mingine sita kwa nia ya kuwezesha taasisi za kifedha kulipwa mikopo kutoka kwa wateja wao ambao biashara zao zimeathiriwa na athari ya janga la COVID-19.

Benki kuu ya Uganda (BOU) katika ilisema katika taarifa kuwa mpango wa hatua hizo unaanza Aprili 1.

Mnamo Aprili mwaka jana Benki hiyo iliweka Hatua za Usaidizi  ikilenga kudumisha utulivu wa kifedha na kupunguza athari za kiuchumi za janga hilo.  

Biashara nyingi ambazo ziliathirika na janga hilo zimetoa wito kwa serikali kuzitaka taasisi za kifedha kurekebisha mipango yao ya ulipaji wa mikopo.