Benki ya Equity yaingia ubia kimataifa
2021-02-19 18:20:25| CRI

Benki ya Equity imetangaza ubia na kampuni kinara katika tasnia ya huduma za fedha duniani ili kurahisisha upokeaji na utumaji wa fedha kwa lengo la kuongeza tija katika huduma hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za Benki ya Dunia za mwaka 2019, Wenyeji wengi wa Afrika mshariki wanaishi nje ya nchi na mara kwa mara hutuma nyumbani fedha nyingi kwa ajili ya uwekezaji na shughuli mbali mbali. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Robert Kiboti, amesema huduma hizo zipo katika vipengele viwili, kwanza ni  huduma za upokeaji  na utumaji fedha  nje ya nchi.

Benki ya Equity inashirikiana na kampuni kubwa za World Remmit, Western Union, Money Gram, Small World, SimbaPay, Transact, Terrapy na Thunes ili kutuma na kupokea fedha kwa nchi zaidi ya 250 duniani.