Pesa za kidijitali zachangia furaha ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China katika sehemu waliopo
2021-02-23 18:31:15| cri

Mwaka huu wakati wa mapumziko ya mwaka mpya wa jadi wa China, sehemu mbalimbali nchini China ziliwahamasisha wananchi kusherehekea sikukuu mahali waliopo bila ya kurudi nyumbani, kwa njia kutoa bahasha nyekundu za pesa.

Ikiwa kundi la kwanza la miji ya majaribio, miji ya Shenzhen, Suzhou, Beijing, na miji mingine imezindua shughuli za kutoa bahasha nyekundu kupitia mtandao wa Internet, hatua ambayo imechangia furaha kwenye sikukuu hiyo.

Katika siku ya kwanza ya mapumziko, bahasha nyekundu zenye thamani ya RMB yuan milioni 30, sawa dola za kimarekani milioni 4.6 zilitolewa mjini Suzhou. Kaunta maalumu zilizinduliwa katika maduka mengi mjini humo, na watumiaji wakionesha nambari ya malipo kupitia simu ya mkononi mbele ya mashine ya POS, waliweza kulipa pesa awlizozipokea kutoka kwenye bahasha nyekundu.

Ran Xin ni mteja mmoja wa Suzhou, aliomba bahati nyekundu kwa kufanya bahati nasibu kupitia mtandao wa Internet, na alifanya manunuzi kwa kufuata maelekezo kuhusu maduka yaliyoorodheshwa.

Kwa wafanyabiashara, kupokea pesa kupitia simu za mkononi hazihitajiwi kulipa ada yoyote, na pia ni njia rahisi zaidi kuliko njia nyingine za malipo.

Mtafiti wa Taasisi ya Fedha katika Chuo Kikuu cha Fudan, Dong Ximiao ameeleza kuwa, hivi karibuni, miji mbalimbali ikiwemo Beijing, Suzhou na Shenzhen, yote imetoa bahasha nyekundu za kidijitali, ili kuhamasisha matumizi, na kukuza soko la matumizi na kupanua mahitaji ya ndani. Pesa hizo si kama tu ziliotolewa kwa wakazi wa kudumu wa miji hiyo, bali pia kwa wakazi kutoka sehemu nyingine ambao wanasherehekea sikukuu, hatua ambayo ilisaidia utekelezaji wenye ufanisi zaidi wa sera ya kuwahimiza wananchi kusherehekea sikukuu katika sehemu waliko bila ya kurudi nyumbani.