Teknolojia ya kutambua nyuso za kima yazinduliwa
2021-02-24 17:13:11| cri

Hivi karibuni watafiti wa Chuo kikuu cha Kaskazini Magharibi cha China wamezindua teknolojia ya kutambua nyuso za kima kwa kutumia teknolojia ya Akili Bandia, kwa ajili ya kuwafuatilia na kuwasimamia maelfu ya kima wa rangi ya dhahabu wanaoishi kwenye eneo la mlima Qinling.

Ikifanana na teknolojia ya kutambua nyuso za binadamu, teknolojia hiyo mpya inaweza kutambua alama maalumu kwenye nyuso za kima wa rangi ya dhahabu, na kumpa kila kima jina na kitambulisho maalumu kwenye database, ili kuwawezesha watafiti kuwafuatilia, kuwalinganisha na kuwatambua wakiwa msituni.

Teknolojia hiyo imeanza kutumika kwa majaribio na imeweza kutambua kima wapatao 200 kwa usahihi wa asilimia 94.

Hivi sasa kima wa rangi ya dhahabu wapatao elfu nne wanaishi kwenye eneo la misitu la mlima Qinling.