Iran yasitisha utekelezaji wake wa hiari wa itifaki ya ziada ya Mkataba wa Kutoeneza Silaha za Nyuklia
2021-02-24 08:51:41| CRI

Iran jana Jumanne ilitangaza kusitisha utekelezaji wake wa hiari wa itifaki ya ziada ya Mkataba wa Kutoeneza Silaha za Nyuklia na kuzuia sehemu ya kazi za Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) za kusimamia na kukagua shughuli za nyuklia za Iran, kutokana na Marekani kushindwa kuchukua hatua za kuiondolea vikwazo Iran ndani ya muda iliopewa.