SOKA: Harambee Stars kupimana nguvu na Sudan Kusini na Tanzania kabla ya kwenda Misri
2021-02-26 16:31:43| cri

Timu ya taifa ya soka ya wanaume ya Kenya, Harambee Stars itapimana nguvu dhidi ya majirani Sudan Kusini na Tanzania kabla ya mechi za kufa au kupona za kuingia Kombe la Bara Afrika (AFCON). Kenya, ambayo imeratibiwa kuanza mazoezi wiki ijayo, itaialika Bright Stars ya Sudan Kusini Machi 13, kasha kucheza mechi nyingine ya kirafiki na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Machi 15 na Machi 18. Michuano hiyo yote ya kupimana nguvu itachezwa nchini Kenya, lakini viwanja vitakavyotumika kwa mechi hizo bado havijatangazwa, ingawa uwanja wa taifa wa Nyayo na ule wa kimataifa wa Kasarani vimetumika hivi karibuni kwa mechi za kimataifa.