Idara ya watumiaji wa Internet kwa simu za mkononi nchini China yafikia milioni 986
2021-03-01 08:52:23| CRI

Takwimu zilizotolewa jana Jumapili na Idara Kuu ya Takwimu ya China kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii kwa mwaka 2020 zinaonesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, idadi ya watumiaji wa mtandao wa Internet nchini China ilifikia milioni 989, na watu milioni 986 kati yao wanatumia Internet kwa simu za mkononi.

Kwa upande wa mapato na matumizi, takwimu hizo zinaonesha kuwa mwaka 2020 wastani wa pato la mkazi ulikuwa ni Yuan 27,540, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.8 kuliko mwaka 2019. Wastani wa matumizi ya mkazi ulikuwa ni Yuan 21,210, kiasi ambacho kilipungua kwa asilimia 4 ikilinganishwa na mwaka juzi.