SOKA: Wamiliki wa Inter Milan wafunga kikosi cha Jiangsu FC
2021-03-01 16:02:59| cri

Wamiliki wa Jiangsu FC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya China (Chinese Super League), wamekifunga kikosi hicho. Kwa mujibu wa wamiliki hao ambao pia wanamiliki kikosi cha Inter Milan kinachoshiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A), maamuzi yao yalichochewa na haja ya kumakinikia biashara nyinginezo baada ya mazingira ya kuendesha soka nchini China kuwa mabovu. Jiangsu walitawazwa wafalme wa Chinese Super League kwa mara ya kwanza Novemba 2020. Hata hivyo, wamekuwa na ugumu wa kuendesha shughuli nyingi za kikosi pamoja na kumudu mishahara ya wachezaji kutokana na gharama ya juu ya matumizi ya fedha. Hii ni baada ya mkataba wao wa Sh78 bilioni kuonyesha mechi za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) moja kwa moja nchini China kati ya 2021 na 2022 kufutwa.