UNOCHA yakabiliwa na upungufu wa fedha za kukidhi mahitaji ya kibinadamu katika jimbo la Tigray, Ethiopia
2021-03-01 09:10:46| CRI

Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa UNOCHA imesema hadi sasa imepata asilimia 58 tu ya dola za kimarekani bilioni 1.3 zinazohitajika kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia.

UNOCHA imeomba wadau kuongeza dola za kimarekani milioni 570.1 ili kukidhi mahitaji ya watu hao. Hadi sasa kuna zaidi ya watu milioni 2.25 wana mahitaji ya kibinadamu katika jimbo la Tigray. Mbali na watu katika jimbo hilo, wakimbizi zaidi ya elfu 61 wa Ethiopia walioko nchini Sudan pia wanahitaji msaada wa kibinadamu.

UNOCHA pia imesema ina wasiwasi na kuwepo kwa vitendo vinavyoripotiwa mara kwa mara vya nyumba kuchunguzwa, uporaji, mauaji na ukatili wa kijinsia katika jimbo la Tigray.