Raia 16 wauawa katika mashambulizi ya waasi nchini DRC
2021-03-01 09:32:53| CRI

 

 

Raia wasiopungua 16 wameuawa kuanzia Jumamosi hadi Jumapili katika mashambulizi kadhaa yaliyofanywa na waasi wa kundi la ADF kutoka Uganda katika jimbo la Kivu Kaskazini na jimbo la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika jimbo la Kivu Kaskazini, raia wasiopungua 10 waliuawa na waasi wa kundi hilo, na katika jimbo jirani la Ituri, waasi wengine wa kundi hilo walishambulia kijiji cha Boyo na kuwaua raia sita. Msemaji wa jeshi la serikali mkoani Ituri Bw. Jules Ngongo, amesema mapambano kati ya waasi hao na vikosi vya Jeshi la DRC (FARDC) yaliendelea mpaka usiku.

Katika miezi kadhaa iliyopita waasi wa kigeni wa Kundi la ADF-Uganda wameendelea kufanya mashambulizi katika majimbo hayo mawili, wakati jeshi la DRC linaloungwa mkono na tume ya Umoja wa Mataifa linafanya operesheni ya kijeshi dhidi yao.