Mkurugenzi mkuu mpya wa WTO aapishwa rasmi
2021-03-01 20:11:43| CRI

Mkurugenzi mkuu mpya wa WTO aapishwa rasmi_fororder_VCG111319359714

Mkurugenzi mkuu mpya wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Bibi Ngozi Okonjo-Iweala ameapishwa rasmi leo tarehe 1 Machi, hivyo kujaza nafasi hiyo iliyokuwa wazi kwa muda wa nusu mwaka.

Bibi Ngozi Okonjo-Iweala ni Mwafrika wa kwanza kuteuliwa kushika wadhifa huo, pia ni mkurugenzi mkuu wa kwanza mwanamke.