Afrika Kusini yapunguza kiwango cha kufunga miji
2021-03-01 16:44:56| cri

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametangaza kuwa, kutokana na kupungua kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona, nchi hiyo imeamua kupunguza kiwango cha kufunga miji kutoka ngazi ya tatu hadi ngazi ya kwanza ambayo ni chini zaidi.

Rais Ramaphosa amesema, wiki iliyopita, idadi ya kesi mpya za maambukizi ya COVID-19 ilikuwa chini ya elfu 10, ikilinganishwa na mwezi uliopita ambapo maambukizi ya virusi hivyo yalikuwa zaidi ya elfu 40 kwa wiki, ikimaanisha kuwa, kilele cha wimbi la pili la janga la COVID-19 nchini humo kimepita.

Rais Ramaphosa pia amesema, mpaka sasa, wahudumu elfu 67 wa afya wamepewa chanjo ya virusi vya Corona.

Habari zinasema, Afrika Kusini kwa sasa imepunguza muda wa marufuku ya kutoka nje usiku, kuruhusu mauzo ya pombe na kuruhusu mikutano.