RAGA: Timu za taifa za Raga za Kenya zafungwa katika fainali za Madrid Sevens
2021-03-01 16:02:30| cri

Timu za taifa za raga ya wachezaji saba kila upande za Kenya Shujaa na Lionesses zilipokea vichapo vikali dhidi ya Argentina na Russia katika fainali ya Madrid Sevens, Jumapili. Shujaa, ambayo ilimaliza duru ya ufunguzi ya Madrid Sevens katika nafasi ya pili Februari 21, ililazimika kukubali nafasi hiyo tena baada ya kuchabangwa 45-7 na Argentina katika fainali ya wanaume. Dakika chache kabla, Lionesses ilikuwa imekung’utwa 19-0 na Russia katika fainali ya wanawake. Mashindano haya ni ya kusaidia timu kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki.