China yaendelea kuongoza duniani kama kituo cha uzalishaji kwa miaka 11 mfululizo
2021-03-01 19:01:09| cri

Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Mawasiliano nchini China (MIIT) imesema, China imedunisha nafasi yake kama kituo kikuu cha uzalishaji duniani kwa miaka 11 mfululizo, ikichangia asilimia 30 ya bidhaa zinazozalishwa duniani.

Waziri wa wizara hiyo, Xiao Yaqing amesema leo kuwa, katika miaka mitano iliyopita, thamani ya bidhaa zilizozalishwa nchini China imeongezeka kutoka dola za kimarekani trilioni 3.63 za kimarekani na kufikia dola za kimarekani trilioni 4.8.

Takwimu zilizotolewa na Wizara hiyo zimeonyehsa kuwa, katika kipindi cha Mpango wa 13 wa Miaka Mitano kilichoanza mwaka 2016 hadi mwaka 2020, kiwango cha ukuaji wa thamani ya nyongeza kutoka sekta ya uzalishaji wa teknolojia ya juu nchini China kilifikia asilimia 10.4, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.9 kutoka lile la uzalishaji wa jumla.