Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China kuanza tarehe 4 mwezi huu
2021-03-01 16:45:52| cri

Kikao cha nne cha Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), kinatarajiwa kuanza Alhamis wiki hii hapa Beijing.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa Kamati Kuu ya Baraza la Mashauriano uliofanyika leo Jumatatu hapa Beijing.

Ajenda zilizopendekezwa kwa ajili ya mkutano huo ni pamoja na kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi za Kamati Kuu ya CPPCC na ripoti ya jinsi mapendekezo kutoka kwa washauri wa kisiasa yalivyoshughulikiwa katika msimu uliopita.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CPPCC wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 13 wa Bunge la Umma la China lililopangwa kuanza Ijumaa, kama washiriki wasiokuwa na uwezo wa kupiga kura.

Wajumbe hao watasikiliza na kujadili miswada mbalimbali ikiwemo ripoti ya kazi za serikali na muswada wa Mpango wa 14 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya China, na Malengo ya Muda Mrefu ya mwaka 2035.