SOKA: Manchester United yashindwa kuitambia Chelsea
2021-03-01 16:03:21| cri

Kocha wa Mchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kwamba baadhi ya maamuzi ya marefa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) uwanjani yanachochewa na “nguvu za nje”. Hii ni baada ya wachezaji wake kulazimishiwa sare ya bila kwa bila na Chelsea katika mchuano ambao mkufunzi huyo raia wa Norway alisisitiza kwamba walinyimwa mkwaju wa penalti. Matokeo ya Man-United katika mchuano huo yaliwapoteza fursa ya kuendelea kufukuzana na viongozi Manchester City kileleni mwa jedwali la EPL msimu huu. Chini ya kocha Pep Guardiola, Man-City sasa wako kileleni kwa alama 62 huku pengo la pointi 12 likitamalaki kati yao na nambari mbili Man-United.