Wizara ya Ulinzi ya China yasema maendeleo ya kijeshi ya China si tishio kwa nchi yoyote
2021-03-01 19:43:03| cri

Wizara ya Ulinzi ya China imesema, maendeleo ya kijeshi ya China hayana lengo la kutawala nchi nyingine, na ukubwa wa jeshi hilo umedumu kuwa alama ya ulinzi wa taifa la China katika zama mpya.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni kupinga tuhuma kuwa China inarekebisha sera yake ya ulinzi kwa kuendelea kujenga jeshi lake na kuchukua msimamo mkali zaidi inaposhughulikia migogoro kati yake na nchi jirani.

Wizara hiyo imesema, China inaendeleza jeshi lake la ulinzi kwa lengo la kulinda mamlaka yake, usalama, na maslahi yake ya maendeleo, na hailengi au kuwa tishio kwa nchi nyingine yoyote.

Aidha, wizara hiyo imesema, katika miaka ya karibuni, jeshi la China limefanya ushirikiano na wenzi wa kimataifa na kutoa mchango mkubwa katika amani na utulivu wa dunia.