TANZANIA: VIKUNDI VYA AKI NA MAMA NA VIJANA VYAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KULIPA MIKOPO.
2021-03-02 18:32:40| cri

Vikundi 66 vya ujasiriamali vijana na wanawake vilivyochukuwa mikopo isiyokuwa na ribakatika halmashauri ya Kahama mkoani Shinyanga, vimefikishwa mahakamani kwa kushindwa kulipa kiasi cha shilingi milioni 68.3.

Fedha hizo zilikopeshwa kwa vikundi hivyo mwaka wa 2013/2014 lakini mpaka sasa vimeshindwa kulipa. Katika mwaka wa kifedha wa 2013/2014, vikundi 10 vilifikishwa mahakamani. Mwaka wa fedha wa 216/2017, vikundi 12 vilivyokopeshwa na kushindwa kulipa, vijana vikiwa 10 na wanawake vikundi viwili huku mwaka wa 2017/2018 vikundi 21 vilishindwa kulipa kiasi cha shilingi milioni 28.3.