RIADHA: Serikali ya Tanzania yatoa wito kwa waandaji wa Kili Marathoni
2021-03-02 16:34:20| cri

Serikali ya Tanzania imetoa wito kwa waandaji na Chama cha Riadha kuwaanda washindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon ili waweze kushiriki mashindano ya Kimataifa ya Olimpiki. Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega, amesema, serikali inataka kuona idadi ya washiriki mbio za Kimaifa za Olimpiki inaongezeka. Ulega ameyataka makampuni yaliyoandaa mashindano ya mbio za Kilimanjaro ikiwemo kampuni ya bia ya Kilimanjaro, Tigo kuwadhamini wanariadhaa hao waweze kushiriki mbio za Olimpiki. Waziri Ulega amesema hayo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi hafla kutoa zawadi kwa washindi mbio za Kilimanjaro Marathon.