Huawei yaunga mkono malengo ya Maendeleo Endelevu ya UN
2021-03-02 18:31:15| cri

 

Kampuni ya Huawei imeunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN SDGs) katika kujenga ulimwengu wa kijani, ubunifu na umoja ikiwa kampuni hiyo ya teknolojia pia inaamini teknolojia inaweza kufanya kazi kama injini ya maendeleo ya binadamu.

Akizungumza katika Mkutano wa masuala ya Ushirikiano, ukuaji na Ufanisi katika masuala ya teknolojia uliofanyika Shanghai, Makamu wa Rais mwandamizi wa Huawei na mjumbe wa bodi Catherine Chen, alisema teknolojia inaweza kuwa injini ya maendeleo ya binadamu, na akatoa wito kwa watu binafsi na wafanyabiashara kufikiria mambo kwa ukubwa zaidi na kutenda kidogo.

Chen alisema ni muhimu kwamba watu wawe  karibu zaidi na teknolojia, ambayo kimsingi inaweza kuwa nguzo sahihi ya kufikia malengo ya maendeleo.

Chen alielezea jinsi Huawei ilivyo tayari kupeleka suluhisho za kidijiti kuwawezesha watu na kufikia malengo ya maendeleo ya UN – haswa malengo ya uvumbuzi, usawa na elimu bora.

Kwa Afrika Kusini, kwa mfano, Huawei, shirika lisilo la faida la Click Foundation waliungana na kuunganisha zaidi ya shule 100 za msingi za mijini na vijijini kwenye huduma za internet. Lengo ni kuongeza ujuzi wa kusoma na kuziba pengo la dijiti kupitia teknolojia.

Nchini Kenya, Huawei ilishiriki katika kujenga Digitrucks, vyumba vya madarasa vinavyotumia umeme wa jua ambavyo huleta ustadi wa kidijiti kwa jamii za pembezoni, ambazo hazina huduma hiyo.