RAGA: Kocha wa Shujaa asema wamepiga hatua kubwa
2021-03-02 16:34:48| cri

Kocha wa timu ya Kenya ya raga ya wachezaji saba kila upande ya wanaume, Innocent Simiyu ameeleza kufurahishwa na hatua ambazo Shujaa imepiga katika maandalizi ya Olimpiki. Namcos alisema vijana wake walicheza vizuri duru mbili za Madrid Sevens, na kuongeza kuwa ameona idara zinazofaa kuimarisha kama jinsi ya kuanzisha mpira na ulinzi. Nchini Uhispania, Shujaa ilikamata nafasi ya pili katika duru ya kwanza ya Madrid Sevens nyuma ya Argentina mnamo Februari 20-21 na pia kumaliza katika nafasi hiyo katika duru ya pili mnamo Februari 27-28. Mbali na Shujaa na Argentina, kitengo cha wanaume pia kilikuwa na Amerika, Ureno, Uhispania na Chile.