KENYA: KQ YAWARUHUSU WASAFIRI KUNUNUA KITI KIMOJA ZAIDI ILI KUIMARISHA USALAMA WAO KIAFYA.
2021-03-02 18:32:13| cri

Wasafiri wanaotumia ndege za KQ na ambao wanazingatia umbali kutoka kwa mtu mwengine, wanaruhusiwa kununua kiti kimoja zaidi karibu nao, kiti ambacho hakitakaliwa na mtu yeyote.

Shirika la ndege la KQ limezindua huduma hii mpya kwa jina Economy Max, kwa wasafiri wanaotaka nafasi zaidi ndani ya ndege kwa ajili ya usalama wao wa kiafya.

Wasafiri wanaruhusiwa kununua kiti kilicho kando yao au kununua safu yote iliyo karibu nao. Wananunua mapema kati ya saa 48 na saa tatu kabla ya kusafiri.

Huduma hii ni ya kwanza kabisa kwa usafiri wa ndege katika bara la Afrika, tangu safari za ndege kurejelewa tena mweiz Agosti baada ya safari zote za angani kusitishwa kwa muda kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.