Ethiopia: Kilimo cha maua chasdaidia kukinga uchumi na kulinda ajira
2021-03-03 19:03:28| cri

Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha wakuzaji na wauzaji wa maua nchini Ethiopia Tewodros Zewdie amesema kilimo cha bidhaa hiyo kimesaidia kukinga uchumi na jamii dhidi ya athari za janga la corona.

Tewodros amesema sekta hiyo inazalisha utajiri mkubwa kwa uchumi wa kitaifa, huku ikitoa fursa kubwa za ajira.

Amesema kuwa licha ya tishio la mwanzo la COVID-19 kwenye sekta hiyo, chama chake kilichukua hatua za kiutendaji na hivyo hakuna mtu aliyefutwa kazi.

Kulingana na wizara ya kilimo ya Ethiopia, nchi hiyo ni mzalishaji na muuzaji mkuu wa maua wa pili kwa ukubwa barani Afrika, baada ya Kenya.