Balozi wa China katika UM afahamisha mafanikio ya China katika kutokomeza umaskini
2021-03-03 17:23:04| CRI

Ujumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa jana umetoa taarifa kuhusu “kuhimiza utekelezaji wa ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu: uzoefu wa kupunguza umaskini wa China”.

Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun amefahamisha mafanikio makubwa ya China katika kutokomeza umaskini, kueleza umuhimu wake kwa maendeleo ya China na dunia nzima, na kutoa uzoefu wa China katika kupunguza umaskini kwa pande zote.

Balozi Zhang Jun amesema, China imekuwa nguvu kubwa katika kazi za kupunguza umaskini duniani, na kuongeza kuwa, mafanikio hayo yamepatikana kutokana na kushikilia uongozi thabiti wa Chama cha Kikomunisiti cha China, kushikilia na kuzingatia maslahi ya watu, kuhamasisha nguvu za pande mbalimbali za kijamii, na kutekeleza mikakati sahihi ya kuwasaidia watu maskini.

Balozi Zhang Jun amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kuzidisha ushirikiano wa kimataifa katika kupunguza umaskini na ushirikiano wa Kusini na Kusini, kuunga mkono kazi za Umoja wa Mataifa, kufanya kazi ya mfuko wa amani na maendeleo kati ya China na Umoja wa Mataifa, kuharakisha kutimiza ufufukaji baada ya janga la COVID-19 na kukabiliana changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.