SOKA: Mourinho asema, Bale bado anategemewa sana Spurs
2021-03-03 15:37:54| cri

Kocha Jose Mourinho wa Tottenham Hotspur amesema, mshambuliaji wake Gareth Bale ana uwezo wa kutamba katika kikosi chochote duniani kwa sasa na wanahitaji sana maarifa yake katika kila mchuano wa msimu huu. Hii ni baada ya nyota huyo kufunga mabao mawili na kuisaidia Spurs kuifunga Burnley 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Magoli mengine ya Spurs katika mchuano huo yalifumwa wavuni kupitia nahodha Harry Kane na kiungo Lucas Moura. Baada ya kuishindia Real Madrid mataji manne ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), mengi yalitarajiwa sana kutoka kwa Bale aliyerejea kambini mwa Spurs mwanzoni mwa msimu huu baada ya kuagana na Real kwa mkopo.