Makombora yashambulia kambi ya majeshi ya kikosi cha Marekani magharibi mwa Iraq
2021-03-03 18:24:32| cri

Makombora yashambulia kambi ya majeshi ya kikosi cha Marekani magharibi mwa Iraq_fororder_2021030317153374359

Makombora aina ya Katyusha yameshambulia kambi ya muungano wa majeshi unaoongozwa na Marekani iliyoko mkoa wa Anbar, magharibi mwa Iraq.

Taarifa fupi iliyotolewa na Kamandi ya Muungano huo imesema, zaidi ya roketi 10 zilishambulia kambi ya jeshi la anga ya Ayn al-Asad mapema leo lakini hayakusababisha madhara yoyote.

Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo.